MISSED CALL YA SHEMEJI 1-2
Like www.facebook.com/Storyzabeka/
Naitwa AIsha najutia niliyoyafanya na kufanyiwa kwenyendoa yangu naandika nikiwa na machungu ndani ya moyo wangu lkn namchukia zaidi dada yangu.
Aisha ni mtoto wa pili kati yake na dada yake wote wazaliwa wa tanga lakini aisha alikuja dara baada ya kupata kaxi ambapo alibahatika kumpata mchumba ambaye baadae akawa mume.Aisha muda mwingi huutumia kutimiza majukumu ya ofisi na kusahau majukumu yake binafsi hali inayozua utata mara kadhaa hasa pale mume anapohitaji huduma muhimu kutoka kwake . dadayake pia alikuja dar baada ya kuchumbiwa na kuolewa lkn mara kadhaa ndia yake ilikuwa ikikumbwa na misukosuko na kukimbilia kujistiri nyumbani kwangu
***
Mara ya tatu, Ime kufika kwa mdogo wake huyo
na kuomba hifadhi baada ya kuachika kwa
mumewe kwa madai mwanamke huyo ‘ana
mdomo sana’ ilikuwa Jumapili jioni ambapo
alipofika alimkuta Beka tu, shemejiye kwa mdogo
wake, Aisha .
“Oooh ! Shemeji , karibu sana mke wangu . Mbona
ghafla kwema huko ?”
“Kwema shemeji, sijui nyie hapa ?”
“Sisi wazima sana. Ila mdogo wako amekwenda
saluni muda si mrefu,” alisema Beka huku
akiingiza begi kubwa kwenye chumba cha
wageni.
Alipotoka chumbani alifikia kukaa sebuleni …
“Enhe shemeji, vipi huko?”
“Da ! Shemeji nyumbani kwangu bwana si
kwema. ”
“Nini tena shemeji?”
“Nimeachwa. ”
“Ha ! Umeachwa ?”
“Ndiyo.”
“Una maana umeachika siyo ?”
“Ndiyo kuachwa shemeji .”
“Kisa nini shemeji?”
“Sijui mwenyewe, jana usiku kaniambia mimi na
yeye basi , hanitaki tena. Sasa nitamlazimisha
shemeji?”
“Watoto ?”
“Amesema anabaki nao kwa vile umri wao
umefikia kuweza kuishi na baba yao pia .”
“Mh !” aliguna Beka huku akijikuna kichwani kwa
ishara kwamba , hakuwa akiwashwa bali ni
mawazo kuhusu sakata la shemeji yake .
Angekuwa analingana umri na mume wa shemeji
yake huyo angempigia simu na kumuuliza
kulikoni lakini sasa umri uliwatofautisha sana.
“Shemeji we pole sana , lakini pia karibu sana,
jisikie hapa upo nyumbani kwako shemeji yangu,
sawa?” alisema Beka huku akisimama na
kumpiga begani kama kumpoza , akaenda
kwenye simu ambayo ilikuwa chaja akampigia
mke wake …
“Aisha , ndoa yako na yangu leo imevunjika ,
nyumbani kaja mke wangu mkubwa, we ulie tu.”
Aisha kwa vile alijua mke mkubwa ni dada yake
Ime, alimuuliza mume wake mbona mgeni huyo
amefika ghafla sana?
“Kuna matatizo makubwa alikotoka .”
“Kama yapi ?”
“Ungekuja basi , maswali gani hayo ?”
“Oke, nakuja. ”
***
Baada ya dakika ishirini na tano, Aisha alifika
nyumbani kwake na kumkuta dada yake
ameshabadili nguo za safari na sasa yu ndani ya
vitenge ambavyo alijifunga viwili , kimoja
kilikatisha usawa wa nido kingine kwenye kiuno .
Jane alimkumbatia dada yake, wakaganda kama
dakika moja nzima huku wakiulizana hali za
watoto na maisha .
“Karibu sana dada. ”
“Haya asante .”
“Kwema kabisa lakini huko ?”
“Si kwema sana mdogo wangu , shemeji
nimeshamsimulia kila kitu kuhusu nitokako. ”
Aisha akamgeukia mume wake na kumwangalia
kwa macho ya kuna nini kwani…
“Ndoa ya shemeji imevunjika !”
“Eti nini ?”
“Ndiyo hivyo mdogo wangu , shemeji yako
kaniacha, kasema hanitaki tena ndiyo nikaamua
nije kwako nipumzike kidogo kabla sijarudi kijijini
kwa wazazi .”
Aisha alilia sana tena sana hasa alipokumbuka
siku ya ndoa ya dada yake huyo ambapo yeye
alikuwa mpambe.
“Sikia nikwambie dada yangu…”
“Nakusikia mdogo wangu …”
“Kaa hapa mpaka utakapochoka , hakuna haja ya
kwenda nyumbani wala kwa nani. Ukisema
uende kwa wazazi utawapa mzigo , mimi
sikushauri hata kidogo. ”
“Mh ! Vizuri mdogo wangu, nilidhani hata nyinyi
nitakuwa nimewapa mzigo .”
“Wala shemeji, usijali kabisa kuhusu hilo ,”
alisema mume wa Aisha , Beka huku akionesha
dalili za uchangamfu wa hali ya juu kwa shemeji
yake huyo , akaingiza na kautani…
“Ungechelewa kuolewa ningekuoa mimi, wala leo
usingepata tabu kama hivi, ” wakacheka wote
mpaka mbavu hawana!
***
Wiki ilipita , awali mtu wa kwanza kuamka ndani
ya nyumba huyo alikuwa Beka , lakini tangu aje
dada wa Aisha yeye ndiye amekuwa mtu wa
kwanza kuamka na kukaa sebuleni akiwa
amewasha tivii , akitokea Beka husalimiana kisha
hutoka kwenye tivii kwenda kufanya kazi
nyingine za ndani ya nyumba hiyo.
Na mara nyingi Beka akimkuta sebuleni, shemeji
mtu huyo humchangamkia sana…
“Ah! Mume wangu huyo ! Umeamkaje baby ?”
“Nimeamka salama mke wangu, vipi wewe na
kuamka kwako ?”
“Mimi sijambo, najisikia nimeshazoea mazingira
ya hapa .”
“Utazoea zaidi maana upo kwa mumeo wa
ukweli,” alijibu Beka akiwa anaachia tabasamu.
***
Usiku wa siku hiyo, Beka na mke wake , Aisha
walitofautiana chumbani, ikawa zogo …
“Mimi nataka nikisema unisikilize, siyo
kujibishanajibishana, we mwanamke vipi ?”
“Vipi kwani vipi , wewe mwanaume vipi ?
Itaendeleaaa
www.facebook.com/Storyzabeka/ like page hii kwa mwendelezo wa story hii nzuri ya MISSED CALL YA SHEMEJI au njoo WhatsApp 0754396084. Utapata ikiwa yote.
Follow on Instagram@Story_za_bekaboy
Ahsante
No comments:
Post a Comment